Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa Sekta ya Afya na TAKUKURU Februari 19, 2026 Mhe. Aswege Enock Kaminyoge, Mkuu wa Wilaya ya Bunda ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi katika warsha hiyo, amewaasa wadau hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU wakati wote kwa manufaa ya jamii inayopata huduma.

Pia amewataka inapobidi waombe msaada wa kufanyiwa uchambuzi wa mifumo ya utendaji kazi ili kubaini mianya ya rushwa iliyopo na kuchukua hatua stahiki mapema.

Aidha aliipongeza TAKUKURU na Menejimenti ya Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda kwa kuwa kielelezo tosha cha ushirikiano wa sekta binafsi na Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa nchini. 

…………….

Dkt. Omari Ramadhan Mzee Mkurugenzi Msaidizi – Udhibiti Rushwa kutoka TAKUKURU, akitoa salamu za Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo Wilayani Bunda.

Dkt. Omari Ramadhan Mzee Mkurugenzi Msaidizi – Udhibiti Rushwa TAKUKURU akisalimiana na Bw. Salum Mtelela Katibu Tawala Wilaya ya Bunda, mara baada ya kuwasili kwenye Warsha ya Wadau wa Sekta ya Afya wilayani Bunda.

Bw. Mohamed Shariff Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mara akitoa shukrani kwa wadau wa Afya kwa ushirikiano wanaouonesha katika Mapambano Dhidi ya Rushwa wilayani Bunda na Mkoa wa Mara kwa ujumla.