Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, amewasili rasmi nchini Tanzania asubuhi ya leo kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kamati Tendaji ya Shirikisho hilo.

‎

‎Mutsepe amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport, Terminal 1, jijini Dar es Salaam.

‎

‎Dkt. Motsepe ataongoza mkutano huo unaotarajiwa kufanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.

‎

‎Mkutano huo unatarajiwa kukutanisha viongozi mbalimbali wa soka barani Afrika kwa ajili ya kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya mpira wa miguu.

‎

‎Kuwa mwenyeji wa mkutano huo ni ishara ya nafasi ya Tanzania katika ramani ya soka barani Afrika, hususan katika kipindi hiki cha maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027.