Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), marehemu Mzee Edwin Isaac Mtei, Nyumbani kwa marehemu Tengeru (Chama), Wilaya ya Arumeru Mashariki mkoani Arusha, Januari 24, 2026.
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Mzee Edwin Issac Mtei.




