Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akitia saini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), marehemu Mzee Edwin Isaac Mtei, Nyumbani kwa marehemu Tengeru (Chama), Wilaya ya Arumeru Mashariki mkoani Arusha, Januari 24, 2026. Dkt. Mwigulu ameongozana na Mkewe Neema Mwigulu.
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi hayo.




