Na John Walter
Umoja wa mashabiki wa vilabu vya soka Tanzania washirikiana na Jeshi la polisi katika ufanyaji wa usafi katika Hospitali ya Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya uhamasishaji katika kuelekea mchezo wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya Moroco michuano ya Afcon hatua ya 16 bora hii leo.
Akizungumza na mashabiki hao Kamanda wa kikosi cha Afya hospitali ya Polisi Kilwa Road Naibu Kamishna wa Polisi DCP Lucas Mkondya amesema hospitali hiyo sio ya polisi pekee bali inatibu wagonjwaa wote ambapo asilimia 75 ni raia wa kawaida huku asilimia 25 ikiwa ni askari.
”Niwashkuru kwa kuja kushiriki nasi kufanya usafi mngeweza kwenda sehemu nyingine lakini mkachagua hapa na sisi mnatupa nguvu sana lakini inatia faraja pia kwa wagonjwa kuona kwamba sio mnakuwa pamoja kwenye michezo wakati wa furaha bali ata wakati wakiwa wagonjwa kama sasa” Dcp Mkondya
Kwa upande wake Polisi Jamii kanda maalumu ya Dar es Salaam Mkaguzi wa Polisi Insp. Christopha Newton amesema michezo ni sehemu ya jamii lakini
pia imekuwa ikitumika katika kutanzua uhalifu na wahalifu
Nae Mwenyekiti wa Umoja wa mashabiki wa vilabu Tanzania Dokta.Mohamed Hamis amesema hatua hiyo ni hamasa katika kuelekea mchezo wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya Moroco katika michuno ya Afcon hatua ya 16 bora
”Tumeamua kuja kufanya usafi katika hospitali yetu ya Kilwa road ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha watu kuiunga mkono Taifa Stars leo hii dhidi ya Moroco,lakini kuwaona wagonjwa na kuwatia neno la faraja ili Mwenyezi Mungu aweze kuwaamsha vitandani warejee katika shughuli zao za ujenzi wa taifa,tunajivunia hospitali hii kwani imekuwa ikiwanufaisha watu wote na sio askari pekee hivyo tunawaomba na wadau wengine kufika katika hospitali hii”




