“Wachezaji wa Taifa Stars wa kwanza ni nahodha wa Timu, Mbwana Samatta, Kushoto kwake ni Idd Suleiman Nado na Mohamed Hussein wakifanya mazoezi wakijiandaa kabla ya mechi dhidi ya Uganda (The Cranes).”
…………….
Kwa takriban miaka 40, Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na ya Uganda (The Cranes) zimekuwa zikikutana mara kwa mara katika mashindano mbalimbali ya soka barani Afrika, hususan katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Kila wanapokutana, pambano lao huwa linabeba uzito mkubwa, presha na hisia kali kutoka kwa mashabiki wa pande zote.
takwimu za kihistoria zinaonesha kuwa Tanzania na Uganda zimekutana takribani mara 22 katika mechi za kimataifa, zikiwemo mashindano ya CECAFA Cup, CHAN, kufuzu AFCON pamoja na mechi za kirafiki. Katika mikutano hiyo, Uganda imekuwa na matokeo bora zaidi kwa muda mrefu.
Taifa Stars imefanikiwa kushinda mechi 5, huku sare zikiwa 4, na Uganda ikishinda mechi 13. Takwimu hizi zinaonesha wazi ubabe wa The Cranes dhidi ya Tanzania, hasa katika mashindano ya kikanda ya Afrika Mashariki.
Aidha, pamoja na takwimu hizo, Tanzania imekuwa ikionyesha mabadiliko chanya katika miaka ya karibuni. Taifa Stars imeanza kupata matokeo muhimu dhidi ya Uganda, hali inayoashiria kuimarika kwa kikosi na kupungua kwa pengo la ubora kati ya timu hizo mbili.
Kwa Upande wao Baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars wametoa maoni Yao kuelekea mchezo huo utakaopigwa hapo baadae Leo Desemba 27,2025 Majira ya saa 12:30 jioni sawa na saa 2:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
“Waganda sio wanyonge, hata sisi pia sio wanyonge” – Bakari Mwamnyeto akizungumza kuelekea mechi ya leo dhidi ya Uganda (The Cranes).
Kwa Upande wake Novatus Miroshi amesema kuwa “Ni ngumu kushinda mchezo lakini ni rahisi, tunafuata maelekezo ya kocha” – Novatus Miroshi
Naye Feisal Salum amesema kuwa “Mchezo utakuwa mgumu…kwa sababu ni dabi na tunajuana sana” – Kiungo wa #TaifaStars, Feisal Salum

(Imeandikwa na Kuandaliwa na Meleka Kulwa – Fullshangwe Media, kutoka Jijini Dodoma)
