Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi na Menejimenti ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) baada ya kuzungumza nao alipokwenda kujitambulisha katika ofisi hiyo jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Menejimenti na Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Capt. Budodi Budodi (aliyesimama) akisoma taarifa ya taasisi hiyo pamoja na maendeleo ya ujenzi wa Karakana ya Wakala ya Ndege za Serikali wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipotembelea taasisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wakwanza kushoto) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Capt. Budodi Budodi (wakwanza kulia). Wa pili kutoka kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray na wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali, Prof. Mhandisi Idrissa Mshoro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akifurahia jambo kabla ya kuzungumza na Menejimenti na Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Regina Qwaray.
Na. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora-Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ameipongeza Bodi, Menejimenti na Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kwa kuongoza na kusimamia Ndege za Serikali kwa weledi na ufanisi mkubwa.
Waziri Kikwete amesema hayo Desemba 12, 2025 jijini Dar es salaam wakati alipotembelea ofisi ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kwa lengo la kujitambulisha.
“Ninaipongeza Bodi kwa kuendelea kuwa washauri wazuri na kufanya uendelevu wa Wakala, binafsi ninaridhika na utendaji kazi wake. Pia Nitumie fursa hii kuwapongeza watumishi wote kwa ustadi wenu mkubwa wa kusimamia Ndege za Serikali, mimi na Naibu Waziri wa ofisi yangu Mhe. Regina Qwaray tunawahakikishia ushirikiano wa dhati wakati wote wa uongozi wetu” alisema Mhe. Kikwete.
Aidha, Mhe. Kikwete amewapongeza kwa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi ambao unaonekana kuridhisha viongozi wanawahudumia. Hivyo, ametoa rai pia kwa watumishi hao kumpa ushirikiano Naibu Waziri Mhe. Regina Qwaray kwa kuwa anamfahamu uwezo wake katika kazi na atasaidia kuongeza ufanisi mara dufu.
Vile vile Mhe. Kikwete amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi ya kuongoza Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo TGFA ni moja ya taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo.
Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray ameahidi kutoa ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya taasisi hiyo muhimu katika Taifa.
“Leo tumekuja kujitambulisha ili tupate kufahamiana kwa kuwa sisi ndio tutafanya kazi pamoja, naomba tuendelee kuwa na ari ile ile ya kufanya kazi kwa ushirikiano ili tuweze kufanikiwa” alisema Mhe. Qwaray.
Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ndege za Serikali Capt. Budodi Nicholaus Budodi alisema kuwa Wakala inaendelea vizuri kusimamia miradi mbalimbali inayoendelea katika ofisi hiyo.
Vile vile, kwa niaba ya taasisi ameahidi kuendelea kuwa wasikivu katika maelekezo wanapata kutoka kwa viongozi na kutekeleza kwa wakati na kwa ufanisi.



