
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke wakiwa katika mbio za TIA Marathon 2025 zilizofanyika leo, Desemba 13, 2025, katika Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Dar es Salaam zikiwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum pamoja na kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.



Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke wakishiriki mbio za TIA Marathon 2025
………….
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke limeungana na taasisi mbalimbali kushiriki mbio za TIA Marathon 2025, zikiwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum pamoja na kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Mbio hizo za TIA Marathoni 2025 zimefanyika leo, Desemba 13, 2025, katika Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Dar es Salaam.
Katika mbio hizo kulikuwa na mbio za mita 5, 10 na 21, huku TANESCO Mkoa wa Temeke wameshiriki mbio za mita 5, 10 kwa lengo la kutoa mchango wa kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum, wakiwemo wakina mama wanaojifungua wakiwa wanaendelea na masomo chuoni.
Mbio za TIA Marathoni 2025 zimebeba kauli mbiu isemayo: “Kimbia, Hamasisha, Saidia.”



