Yanga SC yaibuka na ushindi mwembamba dhidi ya Coastal Union katika pambano la kusisimua la NBC Premier League msimu wa 2025/26.
Katika mchezo uliochezwa mjini Tanga, timu hizo zilionekana kulingana nguvu kwa dakika 45 za kwanza, huku kila upande ukionesha nidhamu ya ulinzi na kufanya juhudi kubwa kutafuta bao la kuongoza bila mafanikio.
Kipindi cha pili kilipoanza, mchezo uliongezeka kasi na mashambulizi ya Yanga SC yakawa ya mara kwa mara, ingawa Coastal Union nao hawakusita kujibu mashambulizi kwa umakini.
Dakika za mwisho zilipoingia, ndipo mshambuliaji hatari wa Yanga SC, Prince Dube, alipoibuka shujaa. alitikisa nyavu katika dakika ya 88, bao ambalo liliamua mchezo. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Dube kufunga, baada ya kutupia wavuni katika mchezo uliotangulia dhidi ya Fountain Gate.
Bao hilo likadumu hadi mwisho wa mchezo, na Yanga SC wakaondoka na pointi tatu muhimu ugenini.



