Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Mabigwa Barani Afrika (CAF Champions League) Yanga SC, leo Novemba 28, 2025 watakuwa na mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya JS Kabylie.
Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Hocine Ait Ahmed, ambako mabingwa hao kutoka Kundi B watashuka dimbani kusaka pointi muhimu.
Kuna orodha ya wachezaji kadhaa ambao watakosekana kwenye mchezo huo dhidi ya Waarabu wa Algeria kutokana na sababu mbalimbali.
Wachezaji hao ni: Beki Kibwana Shomari, Dennis Nkane, Sure Boy, Abdulnasir (maarufu kama Casemiro), Clement Mzize (mshambuliaji), Farid Mussa, Nizar Othman Abubakar.
Yanga SC inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na morali kubwa baada ya kupata ushindi wa bao 1–0 dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco, katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, chini ya Kocha Mkuu Pedro Goncalves.
