Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imeitupa rasmi rufaa ya Guinea dhidi ya CAF na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu mchezo wa kufuzu AFCON 2025 uliochezwa tarehe 19 Novemba 2024.
Guinea ililalamika kwamba Tanzania ilimchezesha mchezaji aliyevaa namba tofauti na ile iliyosajiliwa kwenye orodha ya wachezaji, wakidai kuwa tukio hilo liliipa Taifa Stars faida ya kiufundi na hivyo matokeo yabatilishwe na ushindi wa 3–0 utolewe kwao.
Hata hivyo, CAS imebaini kuwa kosa hilo lilikuwa la kiutawala pekee, halikuathiri mbinu, mwenendo wa mchezo, wala kutoa faida yoyote ya kimkakati kwa Tanzania. Kwa msingi huo, mahakama imeidhinisha msimamo wa awali wa CAF na kutoa uamuzi ufuatao:
Taifa Stars inaendelea na maandalizi ya safari ya kuelekea AFCON 2025 nchini Morocco bila mizengwe ya kinidhamu au masuala ya kikanuni.
Uamuzi huu umeongeza utulivu kwenye benchi la ufundi, ari kwa wachezaji, pamoja na matumaini mapya kwa mashabiki kote nchini, huku malengo ya kufanya vizuri kwenye fainali hizo yakiendelea kupewa kipaumbele.
