Na Happy Lazaro, Arusha
Chuo cha Taifa cha Ulinzi – Tanzania kimewasili Mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya kimafunzo.
Mkuu wa chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania Balozi Meja jenerali Wilbert Augustin Ibuge,Mkuu wa Ujumbe kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi akiwaongoza washiriki wa kozi ya NDC kundi la kumi na nne, wanakitivo,pamoja na wasaidizi katika Ziara ya kimafunzo Mkoani Arusha.
Chuo kina jumla ya washiriki 72 kutoka mataifa mbalimbali 17 ikiwemo Tanzania ambapo mataifa hayo ni pamoja mwenyeji Tanzania, kenya, Uganda, malawi, Namibia, Zambia, Botswana, zimbabwe, Bangladesh, south Africa, India, Egypt, Sierra Leone, Ethiopia,Burundi, Rwanda pamoja na Nigeria.
Mkuu wa.chuo cha Taifa cha ulinzi Tanzania NDC ameambatana na wakufunzi waandamizi elekezi pamoja na washiriki wa kozi ndefu ya 14 ya chuo hicho ambayo ilianza septemba na itamalizika julai 2026.
Aidha amesema malengo ya kuja Arusha ni wanafunzi wao wanafanya mafunzo katika usalama wa Taifa na mikakati.
Balozi Meja jenerali Wilbert Augustin Ibuge,amesema kuwa,kwa sababu usalama wa Taifa unajumuisha sekta zote zinazohusika na maendeleo ya nchi ikiwemo ulinzi na usalama yenyewe.
Amesema kuwa ni kawaida kila mwaka chuo cha Taifa cha ulinzi Tanzania kutembelea Arusha kwani ndio kitovu cha Taifa letu kwenye eneo la la utalii hivyo leo tumeanza hapa kwa kukutana na uongozi wa mkoa.
Amefafanua kuwa ,lengo la ziara hiyo kwa mkoa wa Arusha ni kwa washiriki hao kuweza kuelewa hicho kitovu cha utalii wetu kama Taifa na Arusha ndio kitovu chenyewe katika kuangalia kinaendelea na mikakati yake pamoja na kupata mawazo mbalimbali kwa mkoa kuhusiana na kile wanachoweza kupata kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya nchi yao ikiwemo mawazo na uboreshaji pamoja na tija ambayo wanaiona inaongezeka sana kutokana na uwekezaji mkubwa wa serikali.
RC Makalla amewahakikishia usalama na utulivu maafisa wanaohudhuria mafunzo ya NDC.
Aidha CPA Makalla amewakaribisha Wakuu wa Vyombo vya ulinzi na usalama na Maafisa mbalimbali kutoka nchi 16 za Afrika na nje ya Afrika walio kwenye ziara ya mafunzo ya Chuo cha Taifa cha ulinzi (NDC), akiwahakikishia usalama na utulivu kwa kipindi chote cha siku tano watakachokuwa kwenye mafunzo Mkoani Arusha.
“Mkoa wa Arusha ni Kituo cha Utalii kwa Kanda ya Kaskazini, niwakaribishe sana na mjisikie mpo nyumbani. Arusha inaendelea vyema katika sekta ya utalii na sekta nyinginezo za kiuchumi na imeendelea kuwa salama na tulivu kutokana na ushirikiano mkubwa kati ya wananchi na Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.” amesema CPA Makalla.
Katika Programu hiyo ya mafunzo maarufu kama “Tentative Programme for Economy in Tourism”, Washiriki hao kutoka nchi 16 wanatarajiwa kutembelea maeneo ya utalii ikiwemo Makao Makuu ya TANAPA, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha kwa lengo la kujifunza tamaduni na mazingira mbalimbali ya Jiji hilo muhimu kwa uchumi, Utalii na shughuli nyingine za Kidiplomasia.”amesema CPA Makalla.
Kwa upande wake Col Bhekisile Audrey Mathonsi amesema kuwa kupitia ziara hiyo ya kimafunzo wameweza kujifunza maswala mbalimbali ya utalii na kuweza kubadilishana uzoefu namna ya utendaji kazi wao pamoja na kujifunza tamaduni na mazingira mbalimbali na muhimu kwa uchumi, Utalii na shughuli nyingine za Kidiplomasia.




