Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wameendelea kutamba baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4–1 dhidi ya KMC FC katika mchezo uliopigwa leo, Novemba 9, 2025, kwenye Uwanja wa KMC Complex, jijini Dar es Salaam.
Magoli ya Yanga SC yamefungwa na Max dakika ya 36, Pacome dakika ya 74, huku Boyeli akihitimisha karamu ya mabao kwa kufunga dakika ya 81 na dakika ya 90+3.
Kufuatia ushindi huo, Yanga SC imefikisha jumla ya pointi 10 baada ya kucheza michezo minne, na kuendelea kuweka presha kwa wapinzani wao katika mbio za ubingwa.



