……….…………………..
Wakati viongozi mbalimbali wa kimataifa na wataalamu wa kitarajiwa kukutana katika mkutano wa kimataifa wa kujadili hatua za kukabiliana mabadiliko ya Tabianchi COP30 unaotarajiwa kuanza Novemba 10 hadi 21 huko BELEM BRAZIL, Huku Tanzania ikibeba ajenda mbalimbali ikiwemo koronivia joint work on Agricature.
Mkutano huu ni mwendelezo wa mikutano inayofanyika kila mwaka tangu mwaka 1995 kwa ajili ya kuweka mikakati na hatua mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi, sekta ya kilimo ikiwa ni mojawapo ya shughuli zinazochochea mabadiliko hayo.
Katika kijiji cha Bwigiri, wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, Wakulima wamesimama kwenye ardhi kame, wakitazama mustakabali wao kupitia mbegu bora zinazodaiwa kustahimili ukame teknolojia inayotajwa kama suluhisho la kisasa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Lakini nyuma ya matumaini hayo, kuna simulizi ya changamoto zinazotishia mafanikio ya kilimo cha wakulima wadogo Mbegu Bora, Matumaini Yanayochelewa.
Elisha Mtamwa mkulima wa Bwigiri,anasema kumekuwa na aina nyingi za mbegu lakini makampuni yanayozalisha mbegu hizo yamekuwa yakizalisha mbegu feki hali inayowavunja moyo.
“Mbegu hizi tunazitumia sana lakini changamoto kubwa kwa sasa kuna makampuni mengi wanatuuzia mbegu feki ukipanda hazioti kabisa tunaomba serikali iangalie swala hili kwa undani”Alisema Elisha Mtamwa mkulima kutoka Bwigiri.
Wimbi la Mbegu Bandia Mbwana John, mkulima mwingine kutoka Bwigiri anaongeza kuwa mbegu hizo zinazouzwa kwa nembo za kampuni maarufu ambayo wakulima wanazipenda hali inayowavunja moyo katika kupambana na ukame.
“Kuna makampuni mengine yanachukua nembo ambayo wakulima wameshayazoea nakutengeneza mbegu feki hali hii imekuwa ikiturudisha nyuma”Aliongeza Mbwana mkulima kutoka Bwigiri.
Sio tu mbegu feki wakulima hawa wanasema mbegu hizo, ingawa ni bora zimekuwa zikichelewa kuwafikia wakulima kwa wakati hali inayosababisha wengi wao kushindwa kuendana na msimu.
Ripoti ya FAO (2024) inaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 65 ya wakulima nchini Tanzania hutegemea mvua kama chanzo kikuu cha umwagiliaji. Ukame wa mara kwa mara umeathiri uzalishaji wa chakula, hasa katika mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara.
Mbegu himilivu ni hatua muhimu, lakini FAO inasisitiza kuwa zinahitaji mfumo jumuishi wa utekelezaji umwagiliaji, elimu ya wakulima, na udhibiti wa soko la mbegu.
KUELEKEA COP30 Wakulima wa Bwigiri wanatoa wito kwa serikali na wadau wa maendeleo wanataka sauti zao zisikike situ kama walengwa wa sera bali kama washiriki wa maamuzi,Ruzuku za viuatilifu, mbegu bora zipatikane kwa wakati.
“Kwenye huo mkutano ambao serikali yetu tunaomba watilie mkazo masuala ya ruzuku za viuwatilifu wakulima tumekuwa tukiumia sana mbegu hizi za kisasa zinahitaji kunyunyiziwa dawa mara kwa mara na wakulima wengi wamekuwa wakishindwa kumudu,pia masuala ya uzalishaji wa mbegu bora na zipatikane kwa wakati” Walisisitiza wakulima wa Bwigiri.
COP30 Isikie Sauti za Mashambani Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto halisi kwa wakulima wa Tanzania. Mbegu himilivu ni hatua ya matumaini, lakini mafanikio yake yanategemea uwajibikaji wa serikali, udhibiti wa ubora, na upatikanaji wa rasilimali kwa wakati.



