…………
Afisa Tarafa Lisekese Emmanuel Shilatu amewaongoza Wananchi wa Tarafa ya Lisekese kwenye zoezi la kupiga kura ya kumchagua Rais, Mbunge na Diwani.
Shilatu amekuwa miongoni mwa Wananchi wengi waliojitokeza kupiga kura kwa amani na utulivu.
“Nimeshiriki zoezi la kupiga kura ambapo nimempigia kura Rais, Mbunge na Diwani. Nawapongeza Wananchi wote waliojitokeza kwa wingi kupiga kura na zoezi linaenda vizuri na maeneo yote ya Tarafa hali ya amani na utulivu imeendelea kutawala. Nawapongeza Wananchi wote waliotumia haki yao vyema kikatiba na pia kwa namna walivyoonyesha mapenzi kwa nchi yetu ya Tanzania kwa kudumisha amani na Usalama.” alisema Shilatu mara baada ya kupiga kura.
Nae Mwananchi aliyekuwepo kwenye zoezi la kupiga kura Emmanuel Chilumba amesema wao Wananchi hawawezi kupoteza haki yao ya kimsingi ya Kuchagua viongozi wawatakao watakaowaletea maendeleo.
“Mimi ninaamini viongozi bora wanapatikana kwa sisi Wananchi kujitokeza kuwapigia kura wale tuwatakao. Zoezi lipo vizuri na sisi Wananchi tutaendelea kulinda amani yetu, tutaendelea kuilinda Tanzania yetu.” Alisisitiza Chilumba.
29 Oktoba 2025 Wananchi wenye sifa nchi nzima wanatumia haki yao ya kimsingi ya kupiga kura Kuchagua Rais, Mbunge na Diwani.




