MGOMBEA wa nafasi ya Udiwani Kata ya Kuparang’anda Wilaya ya Mkuranga Mariam Masaninga akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 28, 2025, Mkoani Pwani

……….
MGOMBEA wa nafasi ya Udiwani Kata ya Kuparang’anda Wilaya ya Mkuranga Mariam Masaninga ametumia leo Oktoba 28, 2025 ametoa pongezi kwa mgombea nafasi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha kumaliza kampeni zake kwa amani na utulivu mkubwa.
Masaninga amesema kuwa Mgombea huyo wa Urais ameweza kuzunguka Nchi nzima kwa kufanya kampeni zake na hatimaye leo kufikia tamati.
Masaninga ameyasema hayo leo Oktoba 28 2025. Wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM kata ya kiparang,anda ambapo amesema kuwa mbali na kumpongeza Mgombea urais wa CCM lakini pia anamshukuru Mungu kwa kumaliza salama kampeni zake.
Amesema kuwa ili kuwa ni miezi miwili ya mchakamchaka hekaheka lakini leo tunamshukuru Mungu kwa kufikia tamati leo na matarajio ni makubwa mno kupata ushindi wa kishindo kabisa.
Pia Masaninga amesema kuwa anaimani kubwa mno na wananchi wa kiparang’anda kwamba wameshafanya maamuzi na Oktoba 29 ,2025 wanakwenda kutiki kwa Chama Cha Mapinduzi CCM.
Ameongeza kuwa wananchi wa Jimbo la mkuranga na vitongoji vyake wanaimani na viongozi wao akiwemo Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega kipekee Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
“Naomba sana wananchi wa mkuranga hasa kata kiparang’anda msifanye makosa naamini tumepita kote na tumezungumza mengi mno ya kuhusu Maendeleo lakini Imani yetu mnakwenda kukichagua Chama Cha CCM .”amesema
Amefafanua kuwa kwa mara ya kwanza nchi yetu inakwenda kupata Rais mwanamke wa kuchaguliwa na wananchi wenyewe na Kwa kazi kubwa aliyoifanya ikiwemo ya kuzunguka Nchi nzima Kuomba kura na kunadi Ilani ya CCM niwazi Chama kinakwenda kupata ushindi wa mkubwa sana.
Masaninga amesema kuwa mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa diwani wa kata ya kiparang’anda nikwenda kujenga ofisi ya kata ya CCM kwa kushirikiana na Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Alhaj Abdallah Ulega
Amewaomba wananchi mkuranga kujitokeza kwa wingi na Kwa umoja wao kwenda kupiga kura zote kwa Dkt.Samia Suluhu Hassan .Alhaj Abdallah Ulega ,na yeye Mariam Masaninga kuwa diwani wa kata ya kiparang,anda



