Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya kutoka sare tasa ya bila kufungana dhidi ya Nsingizini Hotspur katika mchezo uliochezwa leo, Oktoba 26, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Kufatia matokea hayo, Simba SC wanasonga mbele wakiwa na jumla ya mabao 3 baada ya mchezo wa awali, miamba hiyo ya soka kutoka Tanzania iliibuka na ushindi mnono wa mabao 3–0 dhidi ya Nsingizini Hotspur ya Eswatini katika mchezo uliofanyika Jumapili, Oktoba 19, kwenye Uwanja wa Mavuso.



