DENIS MLOWE, IRINGA
MJUMBE wa Kamati ya Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa, Salim Abri ‘Asas’ amewataka wananchi kuondokana na hofu ya kujitokeza kupiga kura Oktoba 29 kwa kuwa utakuwa uchaguzi wa amani na utulivu kwa kila mwananchi.
MCC Salim aliongea hayo wakati wa kufunga kampeni za Ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini uliofanyika katika kata ya Isalavanu tawi la Ugute mbele ya maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo.
Alisema kuwa wananchi ifikapo Oktoba 29 nendeni kwenye vituo vya kupiga kwa amani na utulivu na wasikubali kudanganyika na maneno ya kwenye mitandao kwamba kutakuwa na vurugu au maandamano badala yake uchaguzi utakuwa wenye utulivu na amani.
Alisema wasisikilize maneno ya kwenye mitandao inayosambazwa na baadhi ya watu kwani serikali imejipanga vyema kudumisha amani na utulivu oktoba 29 hivyo msihofu kabisa.
Vilevile alisema kuwa anawahakikisha kwamba Mafinga Mji wale ambao hawana elimu ya kupiga kura mtapata elimu hiyo ili jumatano tarehe 29 wote mjitokeze kupiga kura kwa amani na uvulivu upo na kutakuwa na ulinzi wa kutosha na wala hakutakuwa na ghasia nch imetulia kwa kuwa viongozi wako makini.
Alisema kuwa viongozi wetu w mikoa wametuhakikishia amaji , viongozi wa wilaya pia hivyo wananchi mnachotakiwa kwenda kupiga kura kwahiyo nahitimisha kampeni kwa kuwaombea kura wagombea wa Ccm.
“Ndugu zangu hatuna nendeni kupiga kura huu ndio utakuwa uchaguzi wenye amani na utulivu kwenu hivyo msihofu kabisa nawahakikishia hili na nendeni mkakichague chama cha mapinduzi kama ambavyo mmeniahidi hapa” Alisema.
MCC Salim Abri alitumia nafasi hiyo kuomba kura za Rais Dk Samia Suluhu Hassan, mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, mgombea Ubunge wa Mafinga Mjini Dickson Lutevele pamoja na madiwani wote wa kata 9 za Mafinga Mjini.
Alisema kuwa kwanini wananchi wampigie kura Mgombea urais wa CCM, Dk. SamiaSuluhuHassan ni kuhusu kazi na miradi iliyotekelezwa kipindi kilichopita inajitosheleza kabisa kumpa kura za kishindo.
Alisema kuwa wananchi hawana mashaka kabisa na Rais Samia amefanya kazi kubwa na ya kutukika, zawadi kubwa wake kwake kura za kutosha tarehe 29 hivyo narudia tena msihofie kabisa kujitokeza na kupita kura.
Aidha MCC Salim ameahidi kujenga ofisi za CCM za Mafinga kutokana na uchakavu uliokuwa nazo kama zawadi kwa wanaccm wa Mafinga.
Kwa upande wake Mgombea ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini kupitia CCM Dickson Lutevele alisema kuwa maendeleo yaliyofanywa na serikali ya Mama Samia yameonekana na hivyo wananchi wakipigie kura Ccm.
Alisema kuwa wananchi wa Mafinga Mjini wanahitaji maji, Elimu bora, afya na uchumi wao kukua hivyo akichaguliwa atahakikisha anapambania navyo.
Lutevele alisema kuwa katika kumuunga mkono MCC katika kujenga ofisi za Ccm atachangia tani 30 za saruji kwa Ccm ili kiweza kujenga ofisi za CCM wilaya ya Mufindi.




