Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na ujumbe wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Sekretarieti ya Ukanda wa Maziwa Makuu (FP-ICGLR) Ikulu, Zanzibar.
Ujumbe huu unaoongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Domitien Ndayizeye ni sehemu ya utekelezaji wa Itifaki ya ICGLR kuhusu Demokrasia na Utawala Bora, Mkataba wa Umoja wa Afrika juu ya Demokrasia, Uchaguzi na Utawala, pamoja na sheria mpya za Uchaguzi za Tanzania za mwaka 2024.
FP-ICGLR ni miongoni mwa misheni zitakazopeleka waangalizi katika mikoa yote ya Zanzibar kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28 na 29, 2025.




