Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wamefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) baada ya kuichapa Silver Strikers FC ya Malawi mabao 2–0 katika mchezo uliopigwa leo Oktoba 25, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Dickson Nickson Job dakika ya 8, huku Pacome Zouzoua akiongeza la pili dakika ya 34 ya mchezo huo.
Kwa matokeo hayo, Yanga SC inasonga mbele kwa jumla ya mabao 2–1, baada ya kupoteza kwa bao 1–0 kwenye mchezo wa awali uliochezwa nchini Malawi.



