Siraf Maufi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa wakati akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha itete jimbo la Nkasi kaskazini
Mwakilishi wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi CCM UWT Taifa Pili magufuli wakati akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha itete jimbo la Nkasi kaskazini
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Itete waliojitokeza katika mkutano wa kampeni kwa lengo la kusikiliza sera za chama cha mapinduzi CCM
Katika ni mgombea ubunge Jimbo la Nkasi kaskazini Salum Kazukamwe na kulia na mratibu wa uchaguzi kanda ya magharibi Fadhili Maganya.
………………
Na Neema Mtuka, Nkasi
Rukwa:Wananchi wa Kijiji cha Itete kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, ambacho kwa miaka mitano kimekuwa chini ya upinzani, wametakiwa kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuendeleza gurudumu la maendeleo katika eneo hilo.
Akizungumza na leo Oktoba 24,2025 katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha itete jimbo la Nkasi kaskazini Mkoani Rukwa ,
Mwakilishi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Pili Magufuli, ambaye amesema Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mgombea wa Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha sekta ya elimu nchini, hatua iliyowezesha mtoto wa kike kuendelea na masomo hata anapopata changamoto ya ujauzito akiwa shuleni.
Magufuli amebainisha kuwa katika sekta ya nishati, Serikali imejipanga kuboresha mazingira hatarishi kwa kuanzisha mfumo wa nishati safi, unaosaidia kupunguza uharibifu wa mazingira na kulinda usalama wa wanawake, hususani wakati wa kutafuta kuni.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Hajat Ashrafu Maufi, amewataka wananchi wa Itete kukichagua chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya (CCM) katika sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo na afya.
Naye Mratibu wa Kampeni wa Kanda ya Magharibi (mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma), Mjumbe wa Kamati Kuu ya (CCM) na Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Fadhili Rajabu Maganya, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, akisisitiza umuhimu wa kukichagua chama cha mapinduzi kwa kuwa kimeleta maendeleo makubwa nchini.
Aidha,mgombea ubunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini kupitia CCM, Salumu Kazukamwe, akiwa katika kijiji hicho cha Itete, amesema anazitambua changamoto zinazowakabili wananchi wa eneo hilo, ikiwemo uvamizi wa tembo mashambani, ukosefu wa barabara na adha ya mafuriko yanayosababishwa na Mto Kavunja.
Ambapo ameahidi endapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge, atahakikisha changamoto hizo zinatatuliwa kwa vitendo.
Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kijijini hapo akiwemo Edison Makungu amewahimiza wananchi wote kujitokeza kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaowataka bila kurubuniwa na kushawishiwa na mtu yoyote.
“Wananchi wenzangu tujitokeze kupiga kura na tuwachague viongozi tunaowataka kwa maendeleo yetu wenyewe kwani ni haki ya msingi ya kikatiba kupiga kura”.amesema Makungu



