Wahenga husema, “mcheza kwao hutunzwa,” na kweli, kutunzwa huko huwa jambo jema lenye tija. Ndivyo ilivyodhihirika kwa maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi na Zanzibar kwa ujumla, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Asha Rose Migiro walipojitokeza kwa wingi kumtunza na kumheshimu Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ahadi ya kumpa kura nyingi za “ndiyo” zitakazochochea historia mpya ya ushindi mnono wa kishindo.

MCHEZA KWAO HUTUNZWA, DKT. SAMIA AMETUNZWA AHADI YA KURA NYINGI ZA NDIYO



