*Asisitiza safari hii maji yakitoka atakwenda Mahakamani kubadilisha Jina lake.
*Amtaja Dkt Samia Suluhu uwezeshaji wa Maendeleo Jimboni humo.
Na Oscar Assenga, HANDENI
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Handeni Mjini (CCM) Reuben Kwagilwa amesema dhamira ya Serikali ni kulibomoa soko la Chanika wilayani humo na kulijengwa upya ili liwe muonekano na kisasa pamoja na barabara katika mji huo wa Handeni kwa kiwango cha Lami.
Kwagilwa aliyasema hayo Octoba 22 mwaka huu Mjini Handeni katika eneo la Chanika wakati wa mkutano wa hadhara wa Kampeni uliohudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhman ambapo alisema kwamba Serikali ya Dkt Samia Suluhu imewapa kiasi cha Bilioni 15 ambazo Mwenyekiti huyo alisimama na kuzitaja
Alisema fedha hizo zitatumika kwenye ujenzi wa soko hilo ambalo litakuwa la kisasa katika mji huo wa Handeni utakaokwenda sambamba na ujenzi wa barabara za vwango vya lami kata ya Chanika barabara ya kutoka Mahada kwenda Minazini mita 680.
Alizitaja Barabara nyengine kuwa ni ya Rexona mita 130,Barabara ya Melini 110,Barabara ya Shehe Haditi mita 180 ambapo alisema wakimaliza hapo watahamia Kata ya Mdoe watakwenda kuivunja stendi ya Chogo na kujenga stendi ya Kisasa yenye ghorofa juu na chini na inakwenda kuwa stendi bora kuliko stendi zote mkoa wa Tanga na kusini mwa Tanzania.
Akziungumzia mradi wa Mradi wa Maji wa Miji 28 wa (HTM ) alisema kwamba ni mradi wa Kitaifa ambapo kwa upande wa handeni mradi huo umekakamilika kwa asilimia 71 na miezi minne ijayo unakwenda kukamilishwa asilimia 29 iliyobakia na tayari wameshajenga tenki kubwa ambalo limezamishwa chini ya mto pale Mswaha wanapokuchukulia maji wameshalaza mabomba kutoka juu ya mlima wa kilele cha Muhandeni.
Alisemamahali hapo wamejenga tenki kubwa la ukombozi la lita milioni 2 limekamilika kwa asilimia 100 wamelaza maji kutoka Kata ya Mlimani kwenda Kata ya Konje wamelaza kutoa mabomba mpaka Sindeni – Tabora kwenye machujio mpaka Mswaha mahali ambapo wanachukulia maji na tayari wameshakamilisha kazi kwa asilimia 71.
“Mgeukie mwenzako mwambie miezi minne ijayo maji yatatiririka kutoka juu ya kilele cha Mlima Mhandeni yataanzia kwenye Kata ya Chanika maji yatanzia Azimio,Changove,Kivesa,Kwamgumi na yatakwenda mitaa mitano kata ya Chanika, na miezi mine ijayo yatakwenda kata mzima ya Mdoe”Alisema
Alisema kwamba hawataishia hapo maji hayo yatatiririka baada ya hapo yatatiiika na kuifikia kata ya Kibaoni na miezi minne ijao kutoka juu ya Kilele cha Mlima Mhandeni yatakwenda Kata ya Konje wataaanzia Kitulwe na maeneo yote itakapata maji na hatimaye kuendelea kutiririka mpaka Kata ya Kwamagome.
Aliongeza kwamba pia maji hayo yatiririka katika Kata ya Kibeleko Kata, kata ya Kwediamba,Kata ya Kwenjugo,Kata ya Msasa,Kata ya Mlimani mahali ambapo wamejenga tenki kubwa la ukombozi mitaa yote 60 kata zote za Jimbo la Handeni mjini na siku hiyo miezi mine ijayo maji yatakapofika kwenye mitaa yote 60 na kata zote 12.
“Nimewahaidi wana Handeni siku hiyo miezi minne ijayo maji yakifika kwenye mitaa yenu nitaoga hadharani na hicho mnachokishangilia kukiona hamtakiona kwa sababu nitaoga na nguo na mara ya mwisho Handeni mjini na Handeni kwa ujumla kupata mradi mkubwa wa maji ilikuwa mwaka 1974”Alisema
Alisema kwamba enzi hizo mbunge alikuwa Musa Masomo imepita miaka 50 amekuja Rais ambaye kwa leo ni Mgombea Urais wa CCM Dkt Samia Suluhu amekuja ametuwekea mradi mkubwa huo na wanakwenda kuwaletea maji miezi minne.
“Miaka 50 ilyopita baada ya Mbunge Musa Masomo nimefuata mimi Kwagilwa Reubeni “Mamba Lwegwanani”Longwisho naweka nadhiri ya pili nasema miezi mine ijayo maji yakitiririka kwenye maeneo yetu nitakwenda mahakamani kubadilisha jina langu na kutokea siku hiyo nitaitwa Kwagilwa Reuben Santagwa Mamba Laigwanani Longisho Mussa Masomo “Alisema
Awali kizungumza katika Mkutano huo wa Kampeni ambapo alikuwa mgeni rasmi,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman aliwataka wananchi wa Handeni na Taifa kwa ujumla kuwachagua wagombea wanaotokana na chama hicho kutokana na kwamba ndio wazalendo watakaowaletea maendeleo