Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) waliopo nchini.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, na yalilenga kujadili fursa za kuimarisha diplomasia ya uchumi na kijamii baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya.