NA JOHN BUKUKU- MKURANGA
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti zitakazoboresha miundombinu ya usafiri kwa kupanua barabara ya Kilwa Road kutoka Kongowe hadi Mkuranga, pamoja na kujenga stendi kubwa ya kisasa ya mabasi Mkuranga, ili kurahisisha huduma za usafiri na kukuza uchumi wa wananchi.
Ameyasema hayo Oktoba 20, 2025, katika muendelezo wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), akibainisha kuwa miradi hiyo ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kupunguza msongamano wa magari katika barabara kuu za miji mikubwa na kufungua fursa za maendeleo katika maeneo ya pembezoni mwa Dar es Salaam.
Dkt. Samia amesema kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kupanua barabara ya Kilwa Road kutokana na msongamano mkubwa wa magari, sambamba na kujenga barabara ya Mkuranga Mjini hadi Kisiju yenye urefu wa kilomita 40, itakayofungua bandari ya Kisiju na kuchochea biashara ya kimataifa.
Aidha, amebainisha kuwa ujenzi wa stendi kubwa ya mabasi Mkuranga umejumuishwa kwenye ilani ya CCM, huku akipongeza wananchi wa Mkuranga kwa kuonyesha utayari wa kushiriki katika mradi huo kwa kutenga eneo maalum la ujenzi.
Mbali na miradi ya miundombinu, Dkt. Samia amesema Serikali itaendelea kusambaza miundombinu ya umeme vijijini na kuhakikisha kila kaya inapata huduma hiyo muhimu kwa gharama nafuu. Amesema kilichobaki sasa ni kwa wananchi kuunganisha umeme majumbani mwao, huku Serikali ikiendelea kusambaza miundombinu hiyo hadi vitongojini.
Aidha, amebainisha kuwa Serikali itaendeleza programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia TASAF na mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri (asilimia nne wanawake, nne vijana na mbili walemavu).
Amesema pia Serikali itakamilisha miundombinu ya elimu na afya katika ngazi zote za utoaji huduma, ikiwemo ujenzi wa vyuo vya ufundi (VETA) katika wilaya zote na shule maalum za sayansi kwa wavulana na wasichana katika kila mkoa, sambamba na ujenzi wa matawi ya vyuo vikuu.
Dkt. Samia amesema sekta ya afya itaendelea kupewa kipaumbele kwa kukamilisha ujenzi wa zahan.