*Amesema kwa miaka minne ameonesha uwezo mkubwa, ujasiri wa kuongoza nchi
Na Mwandishi Wetu, Kishapu
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndg. Stephen Wasira amesema kazi kubwa aliyoifanya Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha miaka minne na nusu aliyoiongoza nchi, ndiyo inayowafanya Watanzania wampe miaka mingine mitano ya kuongoza.
Amesema kukamilika kwa miradi mikubwa ikiwemo Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR), Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere na Daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo-Busisi) ni ushahidi wa uimara na uwezo mkubwa wa Mhe. Samia Suluhu katika kusimamia maendeleo ya nchi.
Wasira ameyasema hayo leo Oktoba 19, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga, akiwa katika mwendelezo wa mikutano ya kutafuta ushindi wa kishindo kwa mgombea urais wa CCM, Dk. Samia, pamoja na wagombea waliosimamishwa na Chama kuwania ubunge na udiwani.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan alipokea kijiti (ungozi) nchi ikiwa kwenye ujenzi wa miradi mikubwa, Mathalan mradi wa kujenga reli ya Kisasa ya SGR, Mmadi ambao Ndg. Wasira alisisitiza kuwa haukusimamiwa na wazungu, bali na wazawa wakiongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TRC Bw. Masanja Kadogosa.
“Mradi huu haukuwa umefika Morogoro, lakini Kadogosa ametoka ameacha mradi umefika Makutupora kilometa 722 kutoka Dar es Salaam lakini Kadogosa ameondoka ameacha na wakandarasi wanaendelea na kazi hii kutoka Mwanza kwenda Isaka na baadae kufika hadi Kigoma, hata nyie mkienda Mwanza mtaona kazi hii na ipo inayotoka Isaka kwenda Tabora na kutoka Makutupora kwenda Tabora na inatoka Tabora kwenda Kigoma reli pia inatoka Kigoma kwenda Burundi ili watu wa DRC walete madini Dar es Salaam kupitia reli.
“Tunaposema mitano tena, ni mitano ya kazi zaidi,” aliongeza Ndg. Wasira.
Aidha, amesema Dk. Samia amefanya kazi kubwa yenye kutukuka kusimamia ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere hadi kukamilika kwake na kuiwezesha nchi kuwa na umeme wa kutosha