NA DENIS MLOWE, IRINGA
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Iringa Mjini, Fadhil Ngajilo anayewakilisha chama cha Mapinduzi amesema endapo atachaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha kuwa Wagonjwa wa moyo na saratani kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wanapata huduma za kibingwa mkoani hapa.
Ngajilo aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Mlandege, ambapo pia alizungumzia hali ya masoko ya Mwamwindi na Mlandege, akiahidi kushirikiana na wafanyabiashara ili kufufua shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo na suala la michezo hususani kuwa na timu ya ligi kuu.
Alisema kuwa atahakikisha anapambana bungeni ikilazimika hata kupanda juu ya meza kuhakikisha kwamba jimbo la Iringa mjini linapata huduma za kibingwa katika matibabu ya magonjwa ya saratani na moyo kuliko kwenda Dar es Salaam au Dodoma na mikoa ya Nyanda za Juu kuja kupata hapa huduma kuliko kwenda mbali kwani Iringa uko katikati.
Alisema kuwa wakimchagua kuwa mbunge atahakikisha huduma hizo ziwe za kudumu hapa Iringa na mikoa kama Ruvuma, Njombe, Rukwa na Mbeya ije ipate huduma hapa.
Ngajilo aliongeza kuwa kata ya Mlandege haina zahanati ya kata hivyo endapo atachaguliwa atahakikisha anashirikiana na diwani wa kata hiyo kutoka ccm kujenga zahanati ili wananchi wapate huduma katika kata yao.
Fadhili Ngajilo aliwaomba wananchi kujitokeza kwa. Wingi kumpa kura rais Samia kwa kuwa ni bingwa wa maendeleo na kuwahakikishia kwamba watashirikiana kwa asilimia 100 kutekeleza changamoto zote ambazo zinaikabili kata ya Mlandege .
Alisema kuwa kwa upande wa miundombinu watahakikisha barabara ya Lubida itakuwa ya kipaumbele kutengenezwa na barabara nyingine zote zitarekebishwa.
Vile vile alisema kuwa Kazi ya mbunge kuvuta fursa kwa ajili ya wananchi wake hivyo kupitia Soko la Mwamwindi namna pekee ya kulichangamsha kibiashara watu wanapishana wanaingia na kutoka ikifika saa kumi soko kama halipo hivyo endapo akipata nafasi watakaa kuangalia changamoto zinazowakabili ili liweze kurudisha hela iliyowekwa.
“Mimi ni sauti kwa wasio na sauti tukimaliza uchaguzi tutakuwa na kikao wafanyabiashara wote kuweza kuzitatua kwa pamoja kwani Hii ni kata ya wajasiriamali nitahakikisha nitawaunganisha na sekta za kibenki ambazo zina riba nafuu” Alisema.
Alisema kuwa atahakikisha wanapata taasisi zenye kutoa mikopo ya riba nafuu.
kuanzisha mafunzo ya ujasiriamali kwa kata zote za manispaa ya Iringa kuweza kupata elimu husika kwa ujumla katika shughuli mnazofanya na kuwapa ujuzi mwingine ambao utawasaidia kuondokana na fikra za kuajiriwa.