Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeahidi kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa kutumia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO), ili kuongeza matumizi ya teknolojia za ndani, kukuza uchumi na kupunguza gharama za ununuzi wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Said Seif Mzee, akiwa ameambatana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Dk. Mohamed Dhamir Kombo, walipotembelea makao makuu ya TEMDO jijini Arusha.
Dk. Mzee ameisisitiza TEMDO kuongeza uzalishaji wa mitambo ya kuongeza thamani ya mazao pamoja na mitambo ya kutengeneza vifungashio, ili kuwawezesha wajasiriamali wa Tanzania kushindana katika soko na kutimiza malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Dkt. Mohamed Dhamir Kombo, ameiagiza TEMDO kuendelea kuzalisha bidhaa bora na za uhakika kwa bei nafuu, ili kuwezesha wakulima wengi kunufaika kiuchumi kupitia mauzo ya bidhaa zilizoongezwa thamani.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah,amesema ushirikiano huo utaongeza ufanisi katika maendeleo ya viwanda, kuchochea matumizi ya teknolojia za ndani na kukuza uchumi wa Taifa.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TEMDO, Profesa Lazaro Busagala, amesema kuwa taasisi hiyo inazalisha zaidi ya aina 16 za bidhaa, ikiwemo vifaa tiba vya hospitali kama majokofu ya kuhifadhia maiti, vichomea taka hatarishi, na vitanda vya wagonjwa vinavyohitajika kufika Zanzibar, ili kusaidia kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi.
Awali , Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO, Profesa Fredrick Kahimba, amesema kuwa taasisi hiyo inaendelea kubuni teknolojia mbalimbali, ikiwemo zile za sekta ya uvuvi kama mashine za kukausha dagaa na majokofu (cold rooms) ya kuhifadhia samaki, nyama na mbogamboga, kwa lengo la kuendeleza uchumi na kuongeza tija katika sekta ya uzalishaji.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Said Seif Mzee,akizungumza mara baada ya kutembelea Makao Makuu ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha kuangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na taasisi hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah,akizungumza mara baada ya kutembelea Makao Makuu ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha kuangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na taasisi hiyo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Dkt. Mohamed Dhamir Kombo,,akizungumza mara baada ya kutembelea Makao Makuu ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha kuangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na taasisi hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TEMDO, Profesa Lazaro Busagala,akizungumza mara baada ya kutembelea Makao Makuu ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha kuangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO, Profesa Fredrick Kahimba,akielezea jinsi taasisi yake inavyotengeneza bidhaa mbalimbali zenye ubunifu mkubwa wa teknolojia .