Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wamekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Silver Strikers katika mchezo wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa leo, Oktoba 18, 2025, nchini Malawi.
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 76 na Adulu, baada ya shambulizi la kushtukiza lililopelekea kuipatia Silver Strikers ushindi muhimu nyumbani.
Licha ya juhudi za washambuliaji wa Yanga SC akiwemo Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli na walishindwa kuipenya ngome ya wapinzani, huku mashuti yao kadhaa yakidakwa na kipa wa Silver Strikers au kupaa juu ya lango.
Yanga SC sasa inalazimika kushinda katika mchezo wa marudiano jijini Dar es Salaam ili kufufua matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika.