Na Meleka Kulwa -Dodoma
Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtumba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anthony Mavunde, ameendelea na kampeni zake za kunadi Ilani ya CCM katika Viwanja vya Tambukareli, Jijini Dodoma, Oktoba 18, 2025.
Akizungumza katika Mkutano huo, Mavunde amebainisha mpango wake wa kushirikiana na viongozi wa vituo vya usafirishaji, Jeshi la Polisi na mgambo wa jiji kuhakikisha usumbufu kwa bodaboda na bajaji unapungua, Pia, Amesema kuwa atajenga mabanda yeye kivuli katika vituo vyote vya bodaboda na bajaji ndani ya Jimbo la Mtumba kuanzia mwezi Novemba.
Aidha, amebainisha kuwa atahakikisha waendesha bodaboda wanamiliki pikipiki zao badala ya kutumia za mikataba, kupitia mpango maalum utakaosimamiwa na yeye mwenyewe.
Katika kuunga mkono jitihada hizo, Mavunde amechangia shilingi Million10 katika mfuko wa maafisa usafirishaji na kufanya mfuko huo kuwa na jumla ya shilingi million 20 hapo awali aliwahi kuwachangia million 10 katika ufunguzi wa Ofisi za Maafisa Usafirishaji Mkoa wa Dodoma na kuweka mpango wa kuwasaidia bodaboda kununua matairi mapya kwa malipo ya awamu kati ya shilingi elfu nane hadi elfu kumi.
Aidha, amebainisha kuwa ataendelea kushirikiana na wadau wa sekta hiyo kuhakikisha changamoto za usafirishaji zinatatuliwa, sambamba na kusisitiza umuhimu wa amani na ushiriki wa wananchi katika uchaguzi Mkuu.
Mavunde pia amesema kuwa maendeleo ya miundombinu ya Ofisi za maafisa usafirishaji Mkoa wa Dodoma, amesema kuwa Dodoma ni miongoni mwa mikoa michache yenye ofisi bora zilizojengwa kwa juhudi za Dkt. Samia .huku akibainisha kuwa ofisi ya Maafisa Usafirishaji imeboreshwa kwa kujengwa uzio na miundombinu ya kisasa ya kufanyia kazi.
Aidha, Mavunde amewashakuru maafisa usafirishaji, waendesha bodaboda na bajaji kwa ushirikiano waliomuonesha katika kipindi cha utumishi wake tangu alipokuwa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, amesema kuwa wamekuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya sekta ya usafirishaji.
Pia, amewataka wananchi wa Jimbo la Mtumba kujijokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, kwa wagombea wa CCM kwa ngazi ya Urais Dkt. Samia , wabunge na madiwani.