Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Suala la kudumisha Amani ni jukumu la kila Mwananchi anaependa Maendeleo.
Alhaji Dkt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 18 OKTOBA 2025 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu kwa Sala ya Ijumaaa na Dua Maalum ya kuiombea Nchi na Uchaguzi Mkuu iliofanyika Msikiti wa Muembe Shauri ,Mkoa wa Mjini Magharibi.