Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete akitangaza kwa umma amri ya kuhusu kupandishwa kwa kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi nchini leo 17 Oktoba 2025 Dar es Mwenyekiti wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mishahara kwa Sekta Binafsi Dkt. Suleiman Rashid Mohamed akizungumza leo 17 Oktoba 2025 kuhusu namna sekta binafsi ilivyoshiriki kwenye mchakato wa majadiliano kuhusu kupanda kwa kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi sekta binafsi ambapo ambapo ameeleza kuridhishwa na mchakato huo.
Naibu Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Rehema Ludanga akieleza faraja walionayo wafanyakazi wa sekata binafsi baada ya amri ya serikali kuhusu kupandishwa kima cha chini cha mshahara kulikotangazwa leo na serikali jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajili Tanzania (ATE) Suzzane Ndomba- Doran amewataka waajili nchini kujipanga kufanya utekelezaji wa amri juu ya kuongeza mishahara kwa watumishi wa sekta ya umma kwa kuwa chama kilishiriki mchakato huo kupitia maoni yaliyokusanywa kwenye mikoa yote nchini. (Habari na Picha na OWM-KVAU)