*Wananchi wapaza sauti kuishukuru Serikali kwa maendeleo makubwa,
*Wahamasishwa kumpokea Dkt. Samia, kupiga kura kwa amani Oktoba 29.
………….
Rais wa Tanzania na Mgombea Urais kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan kesho Jumatano tarehe 15 atawasili kwenye mkoa wa Kagera kuendelea na ziara ya kampeni kuomba ridhaa ya Watanzania kuongoza Tanzania kwa miaka 5 ijayo.
Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera chini ya Afisa Tarafa wake Ndugu Bwanku M Bwanku imefanya matembezi makubwa ya amani na jogging maalum ya kumpokea Dkt. Samia pindi atakapoingia Kagera hiyo kesho. Matembezi na jogging hiyo yamefanyika kuzunguka Mji mzima wa Kemondo huku mamia ya wana Katerero wakijitokeza kushiriki.
Kagera imepata mafanikio makubwa sana ndani ya miaka 4 ya Uongozi wa Dkt. Samia ikiwemo kupandisha bei ya kahawa kutoka 1000 hadi 5000, kujenga Chuo Kikuu UDSM- Bukoba, kujenga VETA 8 na Hospitali 8 za Halmashauri, kuboresha Bandari ya Kemondo na Bukoba Bilioni 38, Miradi 41 ya Maji, miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara, umeme Vijiji vyote 668 vya Kagera n.k
Matembezi na jogging hii ililenga pia kuishukuru Serikali ya Rais Samia kwa mageuzi haya makubwa ya maendeleo kwenye mkoa wa Kagera ikiwemo na Tarafa ya Katerero iliyopata maendeleo makubwa ndani ya kipindi kifupi.