Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro leo tarehe 11 Oktoba 2025. akiwasili mjini Maswa na kulakiwa na Wananchi wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wakiwa pamoja na Viongozi mbalimbali wa Chama na Jumuiya, kwa ajili ya mapokezi ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye atawasilisha hapo muda mfupi ujao na kuzungumza na wananchi katika kampeni zake za kusaka ikulu
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Migiro ametanguliza salamu za upendo na ujio wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM ambaye pamoja na kuja kusalimia, atanadi ilani ya CCM, Sera na Ahadi zake na kuomba kuwa kwa mafiga matatu.