NA JOHN BUKUKU- LAMADI, SIMIYU
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stanslaus Haroon Nyongo, amesema kuwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu wamepokea kwa furaha kubwa ujio wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye alipita kuelekea Mkoa wa Mara.
Aakizungumza Oktoba 9, 2025, katika mji wa Lamadi Busega mkoani Simiyu mkoani Simiyu katika Wilaya ya Bariadi maesema kuwa wananchi wa Simiyu ni wakarimu na watulivu, na wamejitokeza kwa wingi kumpokea mgombea huyo ambaye anatarajiwa kurejea tena mkoani humo kesho.
Aidha, amebainisha kuwa wananchi wa Simiyu wako tayari kumpa Dkt. Samia kura nyingi za kishindo kutokana na uongozi wake wenye weledi, uzalendo na juhudi kubwa za kuwaletea wananchi maendeleo.
Pia, amesema kuwa Dkt. Samia ni kiongozi mwanamageuzi aliyetoa huduma za kijamii kwa wananchi wake na kupambana kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa ipasavyo. Aidha, amebainisha kuwa Mkoa wa Simiyu umenufaika kwa kiwango kikubwa na fedha za maendeleo zinazotolewa na Serikali katika sekta za elimu, afya, maji, umeme na ujenzi wa barabara za lami.
Amesema kuwa tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanzania miaka 61 iliyopita, haijawahi kutokea mkoa huo kupokea miradi mikubwa ya maendeleo kwa kiwango kilichopo sasa.
Amebainisha kuwa Serikali chini ya uongozi wa Dkt. Samia imeleta mageuzi makubwa katika sekta zote, hali inayoufanya Mkoa wa Simiyu kuonekana kama mkoa ulioendelea licha ya kuwa bado mchanga.
Aidha, amebainisha kuwa wananchi wa Simiyu wana upendo wa hali ya juu kwa Rais Dkt. Samia, wakitambua jitihada zake za kuboresha kilimo cha pamba na sekta nyingine za uzalishaji.
Kuhusu vijana, amesema kuwa Dkt. Samia amekuwa kiongozi anayewashirikisha vijana katika mipango mbalimbali ya kitaifa, ikiwemo maandalizi ya Dira ya Taifa. Aidha, amesema kuwa vijana wanapaswa kuendelea kuwa wavumilivu, kuepuka kushawishiwa na watu wanaotaka kuchafua mazingira ya amani, na waendelee kujifunza stadi na maarifa yatakayowasaidia kujiajiri.
Aidha, amebainisha kuwa Serikali imejidhatiti kuwajengea vijana mazingira mazuri ya amani, utulivu na ajira, huku akisisitiza umuhimu wa kubadilisha mtazamo wa kutegemea ajira na badala yake kujiandaa kujiajiri.
Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bariadi Vijijini, Masanja Kadogosa, amesema kuwa ujio wa Dkt. Samia katika mikoa mbalimbali ni sehemu ya kazi ya kunadi ilani ya CCM kwa wananchi kama mgombea wa CCM na kuonyesha utekelezaji wa ilani ya chama hicho.
Aidha, amebainisha kuwa ujio wa mgombea huyo ni fursa kwa wabunge kueleza utekelezaji wa ahadi walizotoa na mipango ya maendeleo ijayo, ikiwemo miradi ya reli, barabara na huduma za kijamii.
Ameongeza kuwa kwa miaka mitano iliyopita chini ya uongozi wa Dkt. Samia, Mkoa wa Simiyu umepiga hatua kubwa za maendeleo, na kwa ilani mpya ya CCM kuna matarajio makubwa zaidi kwa wakulima na wafugaji kupitia ruzuku za mbolea, chanjo na ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha mazao.
Aidha, amebainisha kuwa wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi ujao kumpigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwani kufanya hivyo ni kuchagua maendeleo, ajira na ustawi wa Taifa.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stanslaus Haroon Nyongo

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bariadi Vijijini, Masanja Kadogosa. 




