Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu, Taifa Stars, imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Timu ya Taifa ya Zambia katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia, uliochezwa leo, Oktoba 8, 2025.
Katika mchezo huo, Zambia walipata bao pekee kupitia kwa mchezaji wao Fashion Sakala katika dakika ya 75 ya mchezo.
Kwa matokeo hayo, Taifa Stars inasalia na pointi 10, ikishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi E.




