PICHA mbalimbali za Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika uwanja wa Ndege kisiwani Pemba
leo Oktoba 08, 2025 kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya Kampeni, kusaka kura za ushindi wa kishindo za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.
Dkt.Nchimbi ataanza mkutano wake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba eneo la Kinyasi -Wete na baadae atafanya mkutano wake mkubwa Mkoa wa Kusini Unguja Jimbo la Chwaka.