Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Ezekiel Mashola akizungumza na Wafanyakazi wa mkoa huo wakati akifungua wiki ya huduma kwa wateja katika hafla fupi iliyofanyika leo Oktoba 6, 2025 katika Ofisi za mkoa huo zilizopo Kurasini, Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Temeke, Lucia Renatus akitoa elimu kwa Wafanyakazi wa mkoa huo kuhusu umuhimu wa wiki ya huduma kwa wateja.
Afisa Rasilimali Watu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke Bi. Chausiku Nchagasi akifafanua jambo katika hafla ya uzinduzi ya wiki ya huduma kwa wateja.
Mhasibu wa TANESCO Mkoa wa Temeke Lucy Mwaisemba akitoa taarifa ya mipango iliyowezekana pamoja na mikakati ijayo ya mkoa huo.
Meneja wa TANESCO Wilaya wa Mbagala Mhandisi Elirehema Makacha akitoa taarifa ya mipango iliyowezekana pamoja na mikakati ijayo ya mkoa huo.
Afisa Usalama Mwandamizi TANESCO Mkoa wa Temeke Bw. Stephen Maganga akitoa taarifa ya mipango iliyowezekana pamoja na mikakati ijayo ya mkoa.
Picha za matukio mbalimbali katika hafla fupi ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Temeke.
…….
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke limezindua Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kuandaa mdahalo uliowakutanisha Wafanyakazi na Wakuu wa Idara kujadili mafanikio na mikakati ya utoaji huduma bora na kwa wakati.
Katika uzinduzi huo Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Temeke kwa kushiriki na Wakuu wa Idara walijadili mipango iliyowezekana na kuweka mikakati ijayo, kupata uelewa wa pamoja kuhusu wiki ya huduma kwa wateja, kupitia makala inayoonesha mipango iliyotekelezwa katika mkoa huo.
Akizungumza leo Oktoba 6, 2025 wakati akizindua wiki ya huduma kwa Wateja uliofanyika Ofisi za TANESCO Mkoa wa Temeke, Kurasini, Dar es Salaam, Meneja wa wa Mkoa huo, Mhandisi Ezekiel Mashola, amesema kuwa Shirika limepiga hatua kubwa katika kutoa huduma bora kwa haraka ambapo awali mteja aliunganishiwa umeme ndani ya siku 60, lakini sasa huduma hiyo inatolewa ndani ya siku 14.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Temeke, Lucia Renatus, aliwaeleza wafanyakazi kuhusu kauli mbiu ya Mpango umewezekana katika kuhudumia wateja na kuwakumbusha kuwa mteja hatakumbuka huduma uliyompatia bali atakumbuka ulivyomfanya ajisikie wakati unampatia huduma.
Maadhimisho hayo yameanza rasmi leo, Jumatatu Oktoba 6, 2025, na yanatarajiwa kufungwa Ijumaa Oktoba 11, 2025, yakihusisha ziara kwa wateja, utoaji wa huduma mbalimbali na zawadi, pamoja na kushiriki shughuli za kijamii.
Wiki ya Huduma kwa Wateja huadhimishwa kila mwaka duniani kote katika wiki ya kwanza ya Oktoba, ikiwa ni fursa kwa taasisi na mashirika kuonesha kuthamini mchango wa wateja kupitia utoaji wa huduma bora, kupokea maoni na kutatua changamoto.
Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni: “Mapango Umewezekana.”