Mikutano ya Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan imepata muitikio mkubwa katika mikoa mbalimbali nchini hali inayoashiria uungwaji mkono na makundi yote katika jamii. Hii inatokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa kipindi kilichopita pamoja na ahadi mbalimbali zilizomo kwenye Ilani mpya ya Chama hicho ambayo imegusa masula ya huduma za afya, maji, umeme vijijini, miundombinu ya barabara vijijini na mijini, pamoja na uchumi. Mikoa ya Tanga Pwani, Kilimanjaro, Arusha na Manyara imepata muitikio mkubwa kufuatia kujitokeza kwa wingi kwa wananchi wa maeneo husika kama inavyoonekana pichani.
MIKUTANO YA DKT. SAMIA YAPATA MUITIKIO MKUBWA MIKOANI
