NA Sophia Kingimali.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof.Ibrahimu Lipumba ametoa wito kwa Tume huru ya Uchaguzi(INEC) kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu za uchaguzi lakini kuhakikisha watamtangaza mgombea alieshinda kutokana na kura walizopiga wananchi.
Pia,ameitaka INEC kusimami Sheria na taratibu za uchaguzi kwani kumekuwa na uvunjifu wa sheria unaofanywa na baadhi ya vyama kwa kukusanya kadi za wapiga kura kwa wananchi hivyo wameitaka INEC kutoa Tamko la wazi kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kukusanya vitambulisho vya wananchi vya kupigia kura.
Wito huo ameutoa October 4,2025 kwenye mkutano wa kampeni wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mbagala Said kinyogoli Prof.Lipumba amebainisha kuwa INEC inapaswa kusimamia taratibu na sheria bila ubaguzi.
”Kuna watu wanavunja taratibu na sheria ,Tume inapaswa kulitamka hili wazi kuna watu wanaenda kukusanya vitambulisho vya kupigia kura,hilo ni uvunjaji wa sheria hivyo Tume itoe tamko la wazi kwamba hakuna anayeruhusiwa kukusanya vitambulisho hivyo na vyombo vya Dola viwakamate wanaofanya kosa hil Huu ni wito wetu nautoa hadharani lakini pia unafuatiwa na barua rasmi tunaipeleka Tume ya Uchaguzi,”Prof.Lipumba ameeleza.
Proffesa amesema taratibu za Uchaguzi bado zina changamoto lakini wamejitokeza kushiriki kwa sababu ya Uzalendo walionao na wana shauku ya kuona nchi inapiga hatua madhubuti za kujenga demokrasia imara kwani wanaamini mchakato wa demokrasia unaenda taratibu.
Aidha Lipumba ameongeza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama havipaswi kushiriki shughuli za kisiasa .
” kwenye mitandao kulikuwa na kauli za hovyo ambazo zingeweza kuleta sintofahamu nashukuru msemaji wa Jeshi alitamka kwamba wanajeshi wamekula kiapo kulinda katiba ya nchi wao hawapaswi kujiingiza katika shughuli za kisiasa.Ni muhimu vyombo vyetu vya Dola visishiriki katika shughuli za kisiasa,”amesema Lipumba .
Vile vile ameeleza kipaumbele katika ilani ya CUF ni Katiba mpya ambayo watahakikisha imepatikana katiba yenye misingi mizuri ya Demokrasia
”Lakini ili tupate katiba inayotokana na maoni ya wananchi ilani yetu ya Uchaguzi inaeleza kwamba Chama cha CUF kikishinda Uchaguzi tutaunda serikali ya umoja wa Kitaifa yenye lengo la kujenga umoja wa taifa letu kwa pamoja tuweze kukamilisha zoezi la kupata katiba yenye misingi imara ya Demokrasia katika nchi yetu”, amesema.
kwa upande wake mgombea ubunge jimbo hili Said Kinyogoli amesema changamoto za mbagala anazifahamu hivyo atakapopata ridhaa atakwenda kushughulikia changomato hizo
Pia mesema kuwa anaendelea na ziara za mtaa kwa Mtaa lengo ni kuwafikia wapiga kura wa Jimbo hilo kirahisi.
Kinyogoli amesema ili kuitengeneza Mbagala wananchi wanapaswa kumpigia kura ili aiboreshe sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Elimu katika Jimbo hilo.
”Serikali inatuambia Elimu ni bure,jambo ambalo sio kweli.Hapa tuna shule katika Jimbo letu inaitwa Mikwame Secondary,ile shule walimu ni wachache yaani walioajiriwa na Serikali hawatoshi kwah hiyo wanachukuliwa Waliimu wa ziada kwa ajili ya kwenda kufundisha hawa walimu wa kukodishwa hawalipwi na Serikali wanafunzi wote wanaosoma Mikwame kila Mwezi wanachangishwa elfu mbili kwa ajili ya kulipa Waliimu wale halafu tunaambiwa Elimu bure katika nchi hii sasa mkinipa ridhaa hili nitalikomesha. Amesema Kinyogoli.