NA DENIS MLOWE, IRINGA
NAIBU Katibu Mkuu Umoja wa Wazazi Tanzania Bara, Kilumbe Shabani Ng’enda amewahimiza wanaccm na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa mgombea wa CCM katika nafasi zote ikiwemo Urais, ubunge na madiwani kwa lengo la kuwaletea maendelelo zaidi.
Aidha aliwataka kuongeza nguvu katika kuomba kura kwa ajili ya mama Samia
Ili aweze kushinda kwa kishindo ifikapo Oktoba 29 mwaka huu.
Ng’enda ameyaeleza hayo katika kampeni za mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini katika kata ya Mivinjeni alipokuwa akiwaombea kura Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan, nafasi ya ubunge Fadhil Ngajilo na udiwani Joseph Sanga.
Alisema kuwa kuna kila sababu ya wananchi kumpa kura za kishindo mama Samia kutokana uongozi wake na mambo makubwa aliyoyafanya kwa kipindi kifupi kuliko watangulizi wake.
Alisema watakuja wagombea wa vyama vingine jaribuni kuwaauliza kama wanajua uongozi au wanavigezo vya kuwa viongozi ila wakumbuke uongozi inahitaji watu waaminifu wenye uwezo, waadilifu kwani si kila kiongozi anafaa kuwa kiongozi bora.
“Watakuja lakini je wana uwezo? Mtu anataka urais hata utendaji kata hajawahi fanya ila kwa upande wa CCM tumejua sifa na uwezo wa Rais Samia kapitia ngazi mbalimbali za uongozi na ubora wake kila mtu anajua ‘,Alisema
Ng’enda alisema kuwa Rais ndio roho ya taifa ana majukumu matatu ambayo ni Mkuu wa nchi kuilinda kusimamia ardhi ya nchi zima kusimamia itumike vyema kwa manufaa ya wananchi ,Mkuu wa serikali huduma zote kwa wananchi lazima azitekeleze kwa manufaa na Ndio amiri jeshi mkuu na kuhoji anakuja mtu hajulikani je ukituingiza kwenye matatizo?
Ccm imekuletea dr Samia Suluhu Hassan
Aliongeza kuwa ilani 2025 hadi 2030 ndani ameahidi ndani ya siku 100 atafanya mambo mawili makubwa bilioni 200 kwa ajili ya mikopo kwa vijana wazee na walemavu na ataanzisha bima ya afya kwa wote kwa watu wasiokuwa na uwezo.
Akizumzungumzia mgombea ubunge wa Iringa mjini Fadhili Ngajilo, Ng’enda alisema kuwa Iringa tumefunga injini mpya ya maendeleo, kijana msomi, haji kujifunza uongozi katika ubunge kwani ni chombo kikubwa kinahitaji mtu makini msomi na msikivu mwenye uvumilivu hivyo mpeni kura za kishindo.
Alisema kuwa Ngajilo Kijana mvumilivu kwani amekwenda mara 3 na bado aliendelea kuwa mwaminifu ndani ya chama Mwaminifu, upendo na anayejitoa kwa watu, mpenda michezo, hivyo Ngajilo akichaguliwa atawaletea raha hapa Iringa na vile mama anapenda wasomi basi atafika mbali sana katika majukumu mengine ya Kitaifa.
Alisema kuwa kiongozi bora ni kuzijua changamoto na kuzileta majawabu hicyo mzigo alionao Iringa mjini anaujua ni mzito kiasi gani na amekubali kuubeba kwa ajili ya wananchi.
Kwa upande wake Fadhili Ngajilo alisema kuwa Ajira za Vijana na Fursa za Kiuchumi atahakikisha anaweka Programu za kuwawezesha vijana na wanawake kupata mikopo midogo kupitia Halmashauri na taasisi za kifedha.
Kuendeleza michezo na sanaa kama njia ya vijana kujipatia kipato na kujiepusha na matatizo ya kijamii na kuifanya Iringa kuwa ya utalii wa michezo.
Atahakikisha huduma za Afya na Huduma za Kijamii kushirikiana na serikali kuhakikisha zahanati na vituo vya afya vinaboreshwa na na dawa za kutosha na kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za mama na mtoto.
