Kaimu Naibu Makamu wa Mkuu wa chuo kikuu cha Tumaini Makumira Prof.Fikeni Senkroro akizungumza katika mahafali hayo jijini Arusha.
Mkurugenzi wa shule hiyo Steven Ndosi akizungumza katika.mahafali hayo jijini Arusua leo
……
Na Happy Lazaro, Arusha .
VIJANA nchini wameshauriwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa ajili ya kujipatia maarifa ya kiuchumi huku wakitakiwa kubadilisha maarifa hayo kuwa chanzo cha kuleta mabadiliko kwenye jamii yao inayowazunguka.
Aidha wametakiwa pia kujipima uwezo wao na kuwa wadadisi kuhusu aina ya maisha wanayotaka kuishi kwani kila hatua kwenye maisha yao inategemea maamuzi yao binfasi.
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha Kaimu Naibu Makamu wa Mkuu wa chuo kikuu cha Tumaini Makumira Prof.Fikeni Senkroro wakati akizungumza na wanafunzi pamoja na wazazi kwenye mahafali ya pili ya wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya mchepuo wa kiingireza ya Sekondari ya Naurey Golden Soils iliyopo mkoani Arusha.
Prof .Senkoro amesema kuwa ,hivi sasa kumekuwepo na mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia kutokana na mambo mengi kubadilika ,hivyo ni jukumu.lao kuhakikisha wanatumia teknolojia iliyopo kuleta mapinduzi na mabadiliko makubwa kwenye maisha yao.
Aidha amewataka wazazi kuhakikisha wanakuwa washauri wazuri wa watoto hao kuhusu aina ya maisha wanayotaka kuwa huku wakiepukana kuwalazimisha badala yake tuwaunge mkono kwenye ndoto zao wanazotaka kuwa wao na sio wanazotoka wazazi.
“Najua nafasi ya mzazi ni muhimu sana lakini pia nyie wazazi msiwalazimishe watoto kusomea ndoto tunazotaka sisi bali.tuwape uhuru wao wenyewe wachague wanataka kuwa nani kwenye maisha yao na kwa kufanya hivyo wataweza kutimiza malengo yao waliyojiwekea.”amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hiyo Steven Ndosi amesema kuwa, shule hiyo ina idadi ya wanafunzi 132 ambapo wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwenye swala la taaluma kutokana na walimu kujituma kwa bidii katika ufundishaji na malezi ya watoto wao .
Ndosi amesema kuwa,uwepo wa maabara za kisasa za sayansi umewezesha wanafunzi kuwa mahiri sana katika masomo ya sayansi na uwepo wa kompyuta za kutosha pamoja na Projeslcta kwenye madarasa yote umekuwa ukiongeza kiwango cha ufaulu hapo shuleni kwa kiasi kikubwa kutokana na kufundisha watoto kisasa zaidi.
Ameongeza kuwa kwa upande wa ufaulu wa.kidato cha pili mwaka 2022 ,2023,na 2024 ambapo watahiniwa wote walifaulu kwa madaraja ya kwanza na mbili ambapo kwa mwaka 2024 kati ya watahiniwa 32 ,waliopata daraja moja walikuwa 16,daraja la pili walikuwa 13 na daraja la tatu walikuwa watatu tu ambapo vijana 29 walijiunga na kidaro.cha tano na watatu walipangiwa vyuoni.
Aidha Ndosi ametaja changamoto inayowakabili hapo shule kuwa ni pamoja ja changamoto ya maji ambapo ameomba serikali ya kijiji na kata iwasaidia kuhakikisha shule inakuwa na mfumo endelevu wa maji kwa ajili ya matumizi ya shule.
Ambapo changamoto nyingine ni mashine ya kutolea kopi kwani iliyopo inalemewa ambapo wazazi wa wahitimu waliazimia kufanya harambee ndogo ya kukusanya angalau shs milioni nne ili kununua.
Aidha ametoa wito kwa wazazi kuendeleza tabia ya kufuatilia maendeleo ya watoto ya watoto wao.mashuleni katika taalumanl na maadili ambapo amewataka kulipa ada kwa wakati ili kuepuka usumbufu usio wa lazima kwa watoto wao.
Ndosi amewataka wahitimu na wanaobakia shuleni hapo kuendeleza nidhani kwani ni msingi wa maendeleo ya sasa na baadaye huku akiwataka kuwa watafiti na wabunifu katika elimu na kusoma kwa bidii na kujiepusha na mambo ya hovyo ambayo yatawaharibia malengo yao.
Kwa upande wa wahitimu Sara Salustian amesema kuwa ,wamesema kuwa , shulw hiyo imewajengea misingi imara ambayo imewawezesha kujifunza masomo mbalimbali kwa vitendo zaidi jambo ambalo litawasaidia kuweza kujiajiri kwa maisha yao ya baadaye.