Akizungumza leo Jumamosi Oktoba 04, 2025 katika viwanja vya CCM Sabasaba wilayani Babati, mkoani Manyara, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mratibu wa Uchaguzi wa CCM kanda ya Kaskazini, Fredric Sumaye, alimhakikishia mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwamba changamoto anazokutana nazo zisimuondoe kwenye mstari.
Amesema kuwa chama ndicho kinachopigwa vita zaidi kuliko mgombea, hivyo vita vinavyoendelea viwe chachu ya kuongeza nguvu kwa Dkt. Samia katika harakati zake za kisiasa.
“wala isikukatishe tamaa badala yake ikupe nguvu, kinachotafutwa ni CCM kuanguka, sasa wanakuta hii CCM haitikisiki basi wanaamua kuhamia kwa mgombea lakini nakusifu sana maana hujamjibu hata mmoja,” alisema Sumaye.
Amewasisitiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, ili kuonesha jinsi chama hicho kilivyo na nguvu.