Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Ndugu. Paul Makonda, amemnadi Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. ๐ฆ๐ฎ๐บ๐ถ๐ฎ ๐ฆ๐๐น๐๐ต๐ ๐๐ฎ๐๐๐ฎ๐ป kwa maelfu ya wananchi wa Arusha Mjini mkoani Arusha waliojitokeza katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid leo tarehe 2 Oktoba 2025.
Ndg. Makonda ameeleza kazi kubwa zilizofanywa na Dkt. Samia ndani ya mkoa wa Arusha zilizoacha alama na matokeo chanya kila kona ya Arusha.
Akieleza kazi hizo, Ndg. Makonda amegusia upanuzi wa uwanja wa ndege wa Arusha ambapo amesema hivi sasa ndani ya Arusha zipo ndege ndogo zenye kutoka Arusha kwenda Nairobi ambapo amesema ni dalili njema ya kuendelea kufungua mkoa wa Arusha na imekuwa kwa mara ya kwanza sasa uwanja huu kupokea ndege kutoka nje ya nchi moja kwa moja tofauti na awali ilivyokuwa wakilazimika kwenda viwanja vingine kupata vibali kabla ya kutoa uwanjani hapo.
Ndg. Makonda ameeleza kuwa upanuzi wa uwanja huo ni fursa kwa wafayabiashara na watalii kutoka nje ya nchi kupunguza gharama na kupoteza muda mwingi ambapo amebainisha kuwa ni hatua kubwa ya kukuza uchumi.
Pia, Ndg. Makonda ameeleza kuwa kupitia maelekezo ya Dkt. Samia, mkoa wa Arusha umefanikiwa kutekeleza miradi iliyokwama kwa miaka mingi ambapo amebainisha kuwa zaidi ya bilioni 64 zimetumika na katika jimbo la Arusha mjini tayari ujenzi wa stendi kubwa na ya kisasa ya mkoa imeanza kujengwa pamoja na soko kubwa la kisasa pia linajengwa.
Vilevile, amesema kuwa wananchi wa Arusha wanafurahia uongozi bora wa serikali ya awamu ya sita inayotokana na CCM kwakuwa kulikuwa na changamoto ya umeme lakini sasa umeme wa rea umepatikana na wananchi wanaunganishiwa huduma kwa shilingi 27,000/= tu jambo ambalo limezidi kupania wigo wa upendo wa Watanzania wote kwa CCM.
Aidha, Ndg. Makonda ametoa shukrani zake za kipkee kwa Mgombea Urais Dkt. Samia kwa kuendelea kumuamini na kuamini katika vijana.
“..๐ฌ๐ช๐ฑ๐ฆ๐ฌ๐ฆ๐ฆ ๐ฏ๐ช๐ฌ๐ถ๐ด๐ฉ๐ถ๐ฌ๐ถ๐ณ๐ถ ๐ฌ๐ธ๐ข ๐ฏ๐บ๐ข๐ฌ๐ข๐ต๐ช ๐ป๐ฐ๐ต๐ฆ ๐ฌ๐ถ๐ฏ๐ช๐ข๐ฎ๐ช๐ฏ๐ช ๐ฏ๐ข ๐ฌ๐ถ๐ฏ๐ช๐ฑ๐ข ๐ฉ๐ฆ๐ด๐ฉ๐ช๐ฎ๐ขย ๐ฌ๐ธ๐ข ๐ฏ๐ข๐ง๐ข๐ด๐ช ๐ป๐ข ๐ถ๐ต๐ถ๐ฎ๐ช๐ด๐ฉ๐ช ๐ฌ๐ข๐ฎ๐ข ๐๐ธ๐ฆ๐ฏ๐ฆ๐ป๐ช ๐ธ๐ข ๐๐๐, ๐ฎ๐ฌ๐ถ๐ถ ๐ธ๐ข ๐ฎ๐ฌ๐ฐ๐ข ๐ธ๐ข ๐๐ณ๐ถ๐ด๐ฉ๐ข ๐ฏ๐ข ๐ฉ๐ข๐ต๐ช๐ฎ๐ข๐บ๐ฆ ๐ฌ๐ถ๐ฑ๐ช๐ต๐ช๐ข ๐ท๐ช๐ฌ๐ข๐ฐ ๐ท๐ช๐ฌ๐ถ๐ฃ๐ธ๐ข ๐ท๐บ๐ข ๐ค๐ฉ๐ข๐ฎ๐ข ๐ฌ๐ถ๐ฏ๐ช๐ณ๐ฆ๐ซ๐ฆ๐ด๐ฉ๐ข ๐ฏ๐ข ๐ฃ๐ข๐ข๐ฅ๐ข๐บ๐ฆ ๐ฌ๐ถ๐ด๐ฉ๐ช๐ฏ๐ฅ๐ข ๐ฌ๐ถ๐ณ๐ข ๐ป๐ข ๐ฎ๐ข๐ฐ๐ฏ๐ช ๐ฏ๐ข ๐ฌ๐ถ๐ณ๐ฆ๐ซ๐ฆ๐ด๐ฉ๐ธ๐ข ๐ต๐ฆ๐ฏ๐ข ๐ฌ๐ถ๐จ๐ฐ๐ฎ๐ฃ๐ฆ๐ข ๐ถ๐ฃ๐ถ๐ฏ๐จ๐ฆ ๐ฌ๐ข๐ต๐ช๐ฌ๐ข ๐ซ๐ช๐ฎ๐ฃ๐ฐ ๐ญ๐ข ๐๐ณ๐ถ๐ด๐ฉ๐ข ๐ฎ๐ซ๐ช๐ฏ๐ช..”
“..๐๐ฌ๐ต. ๐๐ข๐ฎ๐ช๐ข ๐ธ๐ฆ๐ธ๐ฆ ๐ฏ๐ช ๐๐ข๐ฎ๐ข ๐ฎ๐ธ๐ฆ๐ฎ๐ข ๐ด๐ข๐ฃ๐ข, ๐ด๐ช ๐ฌ๐ธ๐ข๐ฃ๐ข ๐ถ๐ฎ๐ฆ๐ด๐ช๐ฎ๐ข๐ฎ๐ช๐ข ๐ท๐ช๐ฌ๐ข๐ฐ ๐ฏ๐ข ๐ฌ๐ถ๐ฏ๐ช๐ต๐ฆ๐ถ๐ข ๐ฌ๐ธ๐ฆ๐ฏ๐บ๐ฆ ๐ฏ๐ข๐ง๐ข๐ด๐ช ๐ฎ๐ฃ๐ข๐ญ๐ช๐ฎ๐ฃ๐ข๐ญ๐ช ๐ญ๐ข๐ฌ๐ช๐ฏ๐ช ๐ฃ๐ข๐ฅ๐ฐ ๐ถ๐ฎ๐ฆ๐ฆ๐ฏ๐ฅ๐ฆ๐ญ๐ฆ๐ข ๐ฌ๐ถ๐ต๐ถ๐ญ๐ฆ๐ข ๐ท๐ช๐ซ๐ข๐ฏ๐ข, ๐๐ถ๐ฏ๐จ๐ถ ๐ธ๐ข ๐ฎ๐ฃ๐ช๐ฏ๐จ๐ถ๐ฏ๐ช ๐ข๐ฌ๐ถ๐ต๐ถ๐ฏ๐ป๐ฆ ๐ฏ๐ข ๐ฌ๐ถ๐ฌ๐ถ๐ญ๐ช๐ฏ๐ฅ๐ข..”