Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa CCM, Ndg. Bulugu Magege, 30/09/2025 amekutana na wafanyakazi wa Mbozi Coffee Curing Company Limited na kuwasisitiza wajibu wao wa kizalendo wa kumpa kura za kishindo Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea wa CCM katika nafasi za Ubunge na Udiwani.
Katika mazungumzo hayo, Bulugu aliwaeleza kuwa Dkt. Samia ni Kiongozi mwenye upendo na watanzania anayejali wakulima na wafanyakazi kwa kuendeleza sekta ya kilimo na viwanda hususani kahawa, ambayo ni uti wa mgongo wa wananchi wa Mbozi na mkoa mzima wa Songwe. Alisisitiza kuwa kura zao kwa Dkt. Samia ni kura za maendeleo ya kweli kwa taifa
Katika ziara hiyo, Bulugu aliambatana na Ndg. Haji Shabani Mwalimu, Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mbozi na Ndg. Noel Donald Mkwemba, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Mkoa wa Songwe. Wote kwa pamoja waliwaeleza wafanyakazi hao kuwa CCM ni chombo pekee cha kuwaletea mustakabali bora na kuwataka watimize ahadi yao ya kumpa ushindi wa kishindo Dkt. Samia ifikapo Oktoba 29, 2025.