Kikosi cha Simba SC kimeendeleza makali yake kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo uliopigwa leo, Oktoba 1, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yalifungwa na Chamou Karaboue dakika ya 44, Rushine De Reuck dakika ya 63, na Selemani Mwalimu aliyekamilisha karamu ya mabao dakika ya 85.
Kwa ushindi huo, Wekundu wa Msimbazi wanafikisha pointi 6 baada ya kushinda mechi mbili mfululizo, hivyo kuongoza msimamo wa ligi.