NA JOHN BUKUKU – TANGA
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ataendelea na kampeni zake leo akitokea mkoani Tanga kuelekea mkoani Kilimanjaro, ambako atafanya mikutano ya hadhara katika miji ya Korogwe, Mombo, Same na Mwanga.
Katika mikutano yake, Dkt. Samia amekuwa akiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 na kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisisitiza kuwa kura ya ndiyo kwa CCM ni msingi wa kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na kutekeleza mipango mipya ya kiuchumi na kijamii.
Amesema Serikali ya CCM imeendelea kuwekeza katika sekta za elimu, afya, nishati, maji na barabara, hivyo wananchi wanapaswa kuendeleza mshikamano na ushirikiano wa kitaifa kwa kumpa ridhaa ili kukamilisha dhamira ya kuwaletea maendeleo endelevu.
Aidha, Dkt. Samia ameendelea kusisitiza kaulimbiu ya kampeni ya mwaka huu ya “Twende Sote, Tukapige Kura, Tuipe CCM Ndio” akiwataka Watanzania kuipa CCM dhamana ya kuendelea kuliongoza Taifa kwa vitendo.