KATIBU wa Itikadi siasa na uenezi wa CCM mkoa wa Arusha Saipulan Ramsey akizungumza na waaandish8 wa habari jijini Arusha kuhusu ujio wa mgombea urais.
Happy Lazaro, Arusha .
KATIBU wa Itikadi siasa na uenezi wa CCM mkoa wa Arusha Saipulan Ramsey amewataka wananchi wa Arusha kujitokeza kwa wingi kumpokea mgombea urais wa CCM ambapo maandalizi yote yamekamilika tayari.
Akizungumza na vyombo vya habari katika Soko namba 68 la Kilombero, mbele ya akina mama wajasiriamali wadogo wa mboga mboga, Ramsey amesema Oktoba 1 2025, mgombea huyo ataingia jijini Arusha na kusimama Usa River, Arumeru, ambapo atazungumza na wananchi.
Kwa mujibu wa Ramsey, siku inayofuata Oktoba 2,2025, Mgombea huyo atafanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Uwanja wa Mpira wa Sheikh Amri Abeid, ambapo wananchi wa Arusha wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi.
“Tutafanya mapokezi ya kishindo na tutawafundisha mikoa mingine namna gani mgombea urais anapokelewa. Tutaiweka rekodi sisi wenyewe na kuivunja sisi wenyewe. Hapa Arusha, mikoa mingine watasoma namba,” alisema Ramsey kwa msisitizo, akipigiwa makofi na akina mama wa soko hilo.”amesema Ramsey.
“Tunamkaribisha kwa mikono miwili kwani huu ni wakati wa wanawake na wananchi wote kuonyesha mshikamano wetu. Tutajitokeza kwa wingi na tutashiriki kikamilifu kumkaribisha kiongozi wetu,” alisema kwa tabasamu huku akishangiliwa na wenzake.”amesema.
Ramsey ameongeza kuwa mapokezi hayo ni sehemu ya kuonyesha mshikamano wa wanaCCM na wananchi wa Arusha kwa mgombea wao, huku akiwataka wananchi wote kuungana kwa pamoja kuhakikisha historia mpya inaandikwa jijini humo.
Aidha Ramsey amewaomba kina mama wa soko hilo kuunda vikundi ili waweze kunufaika na mikopo ya halmashauri, akisisitiza kuwa ni fursa ya kuinua mitaji yao na kukuza biashara ndogo ndogo. Aidha, alimwelekeza mgombea udiwani wa Kata ya Levolosi, lilipo soko hilo, kuhakikisha endapo atashinda nafasi hiyo, atasimamia ipasavyo mikopo hiyo ili akina mama wajasiriamali wanufaike kwa vitendo.
Naye mmoja wa wafanyabiashara Salome Mollel maarufu Mama Mandonga mtu kazi, wanaouza mboga katika soko hilo, amesema wanawake wa Arusha wako tayari kumpokea mgombea urais kwa furaha kubwa alimshukuru rais samia kwa kuwaona na kuwajengea Soko hilo ambapo kwa sasa wanaweza hata kujikimu kwa kipato, nakuahidi kumuunga mkono.
Naye Mwenyekiti wa soko no 68 Bakari Rashidi amesema kuwa, wapo tayari kumpokea Rais Samia na wameahidi kumpa kura za kishindo pamoja na wagombea wake wote ndani ya chama hicho na hiyo ni kutokana na mambo mbalimbali ambayo ameyafanya na yanajulikana.