Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Asha Rose Migiro tayari ameshawasili Pangani kwenye uwanja wa Gombelo mahali ambapo mkutano wa Kampeni wa Dkt. Samia Suluhu Hassan Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utafanyika na yeye kuwahutubia wana CCM na wananchi waliojitokeza kwa wingi ili kumsikiliza.
Rais Dkt. Samia pia anatarajiwa kunadi ilani ya uchaguzi ya CCM 2030 na kuelezea utekelezaji wa ilani ya CCM 2025 ambapo pia atatumia mkutano huo kuomba kupigiwa Kura za ndiyo katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, 2025 nchini kote.