Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuendelea na kampeni zake Leo Septemba 28, 2025, kwa kuhutubia wananchi katika mkutano mkubwa Uwanja wa Sabasaba mjini Kibaha, kabla ya kuelekea Chalinze Msata ambako anasubiriwa kwa shauku na wana CCM wa maeneo hayo na wananchi kwa ujumla